Siku moja baada ya mwanasheria Miguna Miguna aliyesimamia kuapishwa kwa Raila Odinga kuwa ‘Rais wa watu’,  kukosoa uamuzi wa kiongozi huyo wa upinzani kutangaza maridhiano na Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi mwingine wa ngome hiyo, Moses Wetangula amehoji uamuzi huo.

Wetangula ambaye ni mmoja kati ya viongozi waandamizi wa NASA amewaambia waandishi wa habari leo kuwa yeye na baadhi ya viongozi waadamizi hawakujua kama Raila alikuwa anafanya mazungumzo yoyote na upande wa Jubilee hususan Rais Uhuru Kenyatta, hivyo wamepanga kumhoji kuhusu hilo.

“Mimi na wenzangu kuotoka kambi ya NASA tutataka maelezo kutoka kwa Raila kuhusu sababu za uamuzi aliouchukua na kwanini alikutana na Rais Uhuru Kenyatta bila kutufahamisha,” alisema Wetangula.

Hata hivyo, amesema kuwa hatua waliyoichukua ya kufanya maridhiano itasaidia kuwaweka Wakenya pamoja.

Aidha, amesema kuwa ili kuwe na maelewano ya kudumu viongozi wa pande zote wanapaswa kuhusishwa na kufikia muafaka na sio watu wawili ambao walikuwa wagombea.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 11, 2018
Mamlaka ya Mawasiliano yaifungia redio ya Umoja wa Mataifa