Serikali imetenga hadi eka 10 za kilimo kwa ajili ya kila kijana ambapo baadaye ataimiliki na kwamba ipo katika mchakato wa kupokea maombi ya awali ya kundi la kwanza.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akijibu swali la jinsi Serikali inavyowavutia Vijana kwenye Kilimo, upatikanaji ardhi, teknolojia na fedha kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kilimo unaofanyika jijini Dakar nchini Senegal.
Amesema, “Lakini pia mafunzo tumefungua vituo ambapo vijana watapatiwa mafunzo kwa miezi mitatu kabla ya kupewa ardhi na kabla ya kuanza kilimo. Pamoja na hayo masuala ya masoko na upotevu wa Mavuno yanazingatiwa.”