Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema mamlaka hiyo imekamata jumla ya kilo  399.28za dawa za kulevya aina ya bangi katika Kitongoji cha Sokoni, Kijiji cha Chogoali,  Kata ya Iyogwe, tarafa ya Gairo, wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari, imesema ukamataji huo umefanyika kutokana na operesheni iliyofanywa na Mamlaka mkoani humo Desemba 22 mwaka 2022 ambapo watu wawili wanashikiliwa kuhusika na usafirishaji wa kiasi hichocha bangi. 

Misokoto na Bangi.

Aidha, watuhumiwa hao wamekutwa na bunduki mbili aina ya gobole zenye namba MG-188  na MG-148pamoja nangozi ya mnyama anayedhaniwakuwa ni Kakakuona. 

Watafikishwa Mahakamani, baada ya taratibu za kisheria kukamilika na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inaendelea kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini, ili kuhakikisha inadhibiti uzalishaji na  usafirishaji wa dawa za kulevya.

Wafugaji 27 wafariki kwa kulipukiwa na bomu machungani
Watatu washikiliwa kwa mauaji ya Dereva, wizi wa magari