Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (katika picha ya pamoja), na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC, Organ Troika jijini Windhoek.

SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade – FIB, Windhoek wamefanya mkutano hii leo Mei, 2023.

Viongozi wengine katika picha ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Felix Tshisekedi, Rais wa Namibia, Hage Geingob, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa pamoja na Viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwasili nchini Namibia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Troika Plus unaowajumujisha Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinazochangia Vikosi kwenye Force Intervention Brigade (FIB).

Mo Salah afikia rekodi ya Steven Gerrard
Tanzania, Canada kushirikiana utafiti sekta ya Madini