Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Fatuma Omar Latu pamoja na dereva wake aliyetambuliwa kwa jina la Alex.

Vifo hivyo, vimetokewa Septemba 14, 2022 Mkoani Mbeya baada ya gari walilokuwa wasisafiria kugongwa na roli lilifeli breki, ambapo Mkurugenzi huyo alikuwa akishiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa, (ALAT).

Kupitia ukurasa wake wa twitter, Rais Samia Suluhu Hassan ameandika “Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Amin.”

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dkt. Rashid Chuachua jana (Septemba 14, 2022), alithibitisha kutokea kwa ajali na vifo hivyo katika mteremko mkali wa mlima Inyala uliopo eneo la pipe line Wilayani Mbeya.

BMT: Mipango ya Serengeti Girls ipo safi
Kenya: Ruzuku yaondolewa, mafuta bei juu