Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema mifumo ya utoaji haki unaochukua muda mrefu kutatua migogoro ni lazima urekebishwe kwa kuwa ni hatari, huongeza gharama na kuathiri mazingira ya uwekezaji na biashara.
Dkt. Samia ameyasema hayo hii leo Februari mosi, 2023 wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria yaliofanyikaviwanja vya chinangali jijini Dodoma na kusema Serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa haki kwa kupitia upya mifumo ya taasisi husika huku ofisi tano ikiwemo ya Mwendesha Mashtaka (DPP), zikiangaliwa kwa macho mawili.
Amesema, “Taasisi tulizoziweka zilikuwa kama tano hivi, taasisi ya mahakama, Mahakama, Magereza, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Ofisi ya mwendesha mashataka, taasisi kama tano hivi zitakwenda kutupiwa jicho kubwa na tume yetu hii.”
Aidha ameongeaza kuwa, Amesema tume hiyo itafanya kazi kwa miezi minne huku ikiangalia mifumo ya usimamizi wa haki na kuimarisha utatuzi wa migogoro si kwa minajili ya kulinda amani ya Taifa pekee bali kukuza uchumi kwa hatua za maendeleo pia.