Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitataka Wizara kujibu kauli za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa kuhusu utendaji wa Serikali.
Ametoa agizo hilo kwa wizara kwa kile alichokitolea mfano kuwa, amewahi kuibuka mwanasiasa aliyeikosoa Serikali kutumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji, ilhali kuna visima kadhaa vilishachimbwa.
Rais Samia ameyasema hayo wakati wa hotuba yake katika mkutano wa faragha na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC).
“Nimewahi kuona kiongozi wa kisiasa akiilaumu Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta vyanzo vipya vya maji kupeleka kwa wananchi, ilhali kuna visima kadhaa vilichimbwa nyuma na serikali iliviacha’
“Wizara inayohusika na hili, ilipaswa kusimama haraka kujibu kutoa facts (ukweli), fugures (takwimu) na kumueleza kwanini visima hivyo viliachwa na kwamba vimeachwa au havikuachwa,” amesema.
“Wizara inayohusika na hili, ilipaswa kusimama haraka kujibu kutoa facts (ukweli), fugures (takwimu) na kumueleza kwanini visima hivyo viliachwa na kwamba vimeachwa au havikuachwa,” amesema.
Aidha Rais Samia amesema kuwa visima vilivyotajwa na mwanasiasa huyo ndiyo vilivyoisaidia Dar es Salaam wakati wa changamoto ya ukame.