Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotumia maafisa habari binafsi, bali wazingatie utaratibu wa kuwatumia maafisa wa vitengo vya mawasiliano serikalini.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi hao pamoja na makatibu na manaibu katibu katika kikao maalum kilichofanyika jijini Arusha.

“Ninafahamu kuwa kila wizara ina kitengo cha habari. Vitengo hivi vinatumikaje, vipo tu vimekaa havifanyi kazi, lakini bado mawaziri maafisa habari wenu wa binafsi wa kutoa taarifa zenu na sio taarifa za Serikali. Hili tukalirekebishe,” amesema Rais Samia.

Rais ametoa agizo hilo alipokuwa akielezea kuhusu umuhimu wa kutoa ufafanuzi juu ya masuala ambayo yanaibuliwa na baadhi ya watu, akitoa mfano wa mwanasiasa aliyelaumu kuhusu uamuzi wa Serikali kutafuta vyanzo vipya vya maji jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa taarifa ya mwanasiasa huyo haikuwa na ukweli, na kwamba ilibidi wizara husika itoe ufafanuzi kwa kutoa ukweli na kwa takwimu.

Aucho awatoa hofu mashabiki
Rais Samia azitaka Wizara kujibu hoja