Rais Samia Suluhu Hassan, amezindua Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City jijini Dodoma, huku akiwataka majaji na mahakimu kutokimbia majukumu ya kutoa haki.

Rais Samia amesema kuwa “Mafanikio hayawezi kupatikana endapo wasimamizi na wadau wa mfumo wa utoaji haki nchini hawatafanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kuongozwa na nafsi katika kufanya kazi na maamuzi”.

“Tumesikia idadi kubwa kata na tarafa ambazo hazina Mahakama na kwa kweli ni kunyima haki wananchi kwahiyo Serikali na wadau tutaangalia tutajitahidi kuhakikisha tunafika kwenye maeneo hayo,” amesema Rais Samia

“Pamoja na ujezi wa vituo jumuishi vya utoaji wa haki, kuongeza idadi ya majaji na mahakimu, kuanzisha mahakama zinazotembea na kuimarisha matumizi ya Tehama hatuwezi kupata mafanikio endapo mahakimu, majaji hawataongozwa na roho njema katika utoaji wa haki,”

“Tuhakikishe haki kwa wananchi inapatikana vile inavyopaswa pia ninatoa rai kwa mahakama kushughulikia suala la ucheleweshwaji wa kesi,”

Aidha ameongeza kuwa “Niwasihi sana mlipe kipaumbele suala la kusikiliza kesi haraka, msikubali kirahisi kubadilisha mahakimu au tarehe za kusikiliza kesi kwasababu hii ni moja ya sababu inoyosababisha kesi zichelewe,” – Rais Samia

“Niwaombe sana Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi muangalie usimamizi wa ubora wa maamuzi kwenye mahakama za mwanzo, malalamiko mengi ya mahakama yanahusu mahakama za mwanzo, kule kutupiwe jicho vizuri,” amesema Rais Samia

KMC FC yaanza kuiwinda Young Africans
Watanzania watakiwa kubadili mitazamo kuhusu katiba