Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan amewataka wasanii wa muziki nchini kuwatungia nyimbo za hamasa timu ya Serengeti girls iliyofuzu kwenda kwenye mashindano ya dunia Oktoba mwaka huu nchini India.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 05, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 17 ( Serengeti Girls) na kuipongeza kwa kufuzu kucheza Kombe hilo.

Amesema kuwatungia nyimbo zenye hamasa zitasaidia kuwapa moyo na kuwajengea uzalendo wa kufanya vizuri wakiwa kwenye mashindano hayo.

Katika hafla hiyo ambayo Mhe. Rais aliwakaribisha rasmi kwenye chakula cha mchana na kuwapa zawadi, amewataka wachezaji hao kujiandaa vema kuelekea katika mashindano ya dunia huku akisisitiza kufanya mazoezi na kuzingatia lishe.

Tukio hilo limepambwa na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya akiwemo Barnaba na Frida Amani ambao waliotumbuiza kwa jumbe nzuri zilizomfanya Mhe. Rais kuwatunza.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu. Dkt, Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu, Menejimenti ya Wizara na wadau mbalimbali wa michezo.

Kiswahili lugha rasmi Uganda
Hersi Said: Fiston Mayele hauzwi NG'O