Rais wa Marekani, Donald Trump ameonywa na wanachama wa chama chake cha Republican kuacha kuingilia uchunguzi maalumu kuhusiana na Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliopita.
Hatua hiyo ya wanachama wa Republican imekuja mara baada ya rais Trump kumshambulia mkurugenzi wa FBI kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya Urusi kudaiwa kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016.
Katika ukurasa wake wa Tweeter mwishoni mwa juma, Trump alitoa utetezi wake kuwa hakukuwa na uhusiano wowote kati ya timu yake ya kampeni na Urusi na kusema kuwa hiyo ni vita binafsi inayoshabikiwa na Democrats.
Hata hivyo, Seneta Lindsey Graham kutoka Republican amemtaka Trump asijaribu kuingilia hatua yoyote dhidi ya uchuguzi huo.