Rais mstaafu, Benjamin Mkapa amesema kuwa elimu ya Tanzania hasa kwa shule za umma ni janga linalolotakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

Mkapa ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ameyasema hayo jana katika hafla ya kumuaga makamo mkuu wa chuo hicho, Profesa Idris Kilula.

“Nimeendelea kusoma sana magazeti mpaka mke wangu ananilalamikia. Lakini barua nyingi za wasomaji zinalalamika zinasema hivyo hivyo. Zinasema elimu ina mushkeli,” alisema.

Mkapa alionesha kusikitishwa na hali ya ufaulu ya shule za umma kwa kulinganisha na shule binafsi na kueleza kuwa kinachohitajika ni mapinduzi katika sekta ya elimu.

“Ninaamni kwamba tuna janga. Ninasoma katika magazeti, ninaletewa mawasilisho kutoka sekta binafsi, walimu, vyuo vikuu binafsi. Napata minong’ono kutoka kwa vyuo vya umma kwamba kuna janga katika elimu,” aliongeza.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, anashauri kufanyika kwa mjadala kujiuliza kama kuna tatizo na kama lipo na jinsi gani linaweza kusahihishwa.

Manara: Hatutakuwa wazalendo kwa Yanga
Rais Trump awekwa kikaangoni