Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa nchi huru za Afrika (AU) akipokea kijiti kutoka kwa rais wa Rwanda, Paul Kagame
Akihutubia umoja huo nchini Ethiopia, Abdel Fattah al-Sisi amesema kuwa atajikita zaidi katika kuimarisha masuala ya kiusalama na kudumisha demokrasia.
Aidha, kuchaguliwa kwake kumehitimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye amemaliza muda wake wa uongozi ndani ya AU.
Hata hivyo Shirika la Kimataifa la Amnesty International limeonya kuwa kuchaguliwa kwa Abdel Fattah al-Sisi kunaweza kudidimiza haki za binadamu.
Tangu mwaka 1995 viongozi wa Misri hawakuwa wakihudhuria mikutano ya AU baada ya jaribio la kuuawa kwa aliyekuwa Rais wake wa wakati huo, Hosni Mubarak.