Mkutano wa Kimataifa unaokusudia kusaka suluhu ya mzozo unaoikabili Venezuela umefunguliwa Montevideo nchini Uruguay wakati rais Nicolas Maduro na mpinzani wake, Juan Guaido wakivutana kuhusu kuruhusu misaada ya kiutu.

Mkutano huo una lengo la kusaka suluhu ya mzozo unaoikabili Venezuela, wakati ambapo rais Nicolas Maduro na kiongozi wa upinzani Juan Guaido wakivutana kuhusu kuruhusu misaada ya kiutu kuingia nchini humo.

Umoja wa Ulaya pamoja na mataifa matano ya Amerika ya Kusini yamekutana katika mji mkuu wa Uruguay, Montevideo kwa lengo la kuandaa mazingira ya mchakato wa kisiasa wa amani.

Aidha, mpango huo ambao awali ulizinduliwa na Mexico na Uruguay kama mkutano wa mataifa yasiyoegemea upande wowote kwenye mzozo huo wa Venezuela, ambapo kwasasa umebadilika na kuwa mkutano wa kundi la mawasiliano lililozinduliwa na Umoja wa Ulaya mwishoni mwa mwezi uliopita, ambapo Costa Rica, Bolivia na Ecuador pia ziliungana na kundi hilo.

Kwa upande wake rais Nicolas Maduro ambaye hakukubaliana na muda aliopewa na Umoja wa Ulaya wa kuitisha uchaguzi wa mapema, aliukaribisha uamuzi wa kufanyika kwa mkutano huo na kuelezea uungaji wake mkono wa juhudi za kufanikisha majadiliano hayo.

Hata hivyo, Guaido, aliyejitangaza kuwa ni rais wa mpito Januari 23 na sasa akitambuliwa na mataifa 40, amepingana vikali na mazungumzo yoyote na serikali, akisema ni namna anayotumia Maduro kupoteza muda.

 

Janga la Mimba Mashuleni laukumba Mkoa wa Kigoma
Video: Bunge kusimamisha mshahara wa Lissu, Serikali yafunguka nyongeza mishahara

Comments

comments