Matokeo ya Sare dhidi ya AS Real Bamako na Ushindi dhidi ya TP Mazembe yamempa jeuri Rais wa Young Africans Injinia Hersi Said, ambaye ametamba kuendelea kuchekelea katika michuano ya Kimataifa.

Young Africans ililazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya AS Real Bamako ugenini nchini Mali, ikitangulia kushinda 3-1 dhidi ya TP Mazembe nyumbani Dar es salaam.

Injinia Hersi amesema: “Young Africans kwa hivi sasa tumefika levo kubwa ya kupata matokeo mazuri popote, iwe nyumbani au ugenini na hicho ndio kitu tunachokitaka.”

“Tunataka kuona timu yetu inapata ushindi popote bila ya kuangalia ukubwa wa timu tunayokutana nayo katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kama tulivyopata matokeo mazuri dhidi ya TP Mazembe.”

“Kabla ya kucheza dhidi ya Mazembe mengi yalizungumzwa, lakini mwisho wa siku tukawafunga mabao 3-1 hapa nyumbani. Tukaenda kupata matokeo ya sare ugenini tulipocheza na Real Bamako. Hivyo wanayanga wawe na imani na timu yao.” amesema Hersi

Young Africans itakuwa mwenyeji wa AS Real Bamako Jumatano (Machi 08), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku US Monastir ya Tunisia itakuwa nyumbani kuikaribisha TP Mazembe ya DR Congo.

Msimamo wa Kundi D, unaonyesha US Monastir inaongoza kwa kuwa na alama 07, ikifutiwa na Young Africans yenye alama 04, huku TP Mazembe ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 03 na AS Real Bamako inaburuza mkia kwa kuwa na alama 02.

Inonga akiwasha Simba SC, ambwaga Kapombe, Mzamiru
Aucho awatoa hofu mashabiki