Beki wa Kati kutoka DR Congo Henock Inonga Baka, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Februari (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Inonga ametangazwa kuwa mshindi wa Tuzo hiyo, kupitia vyanzo vya habari vya Simba SC akiwashinda Beki wa Kulia Shomari Kapombe na Kiungo Mkabaji Mzamiru Yassin ambao aliingia nao Fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Mwezi Februari, Inonga alicheza michezo yote mitano, mitatu ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na miwili ya Ligi Kuu sawa na dakika 450 akifunga bao moja.

Inonga amepata kura 498 sawa na asilimia 57.97, akifuatiwa na Kapombe aliyepata kura 246 sawa na asilimia 28.64 na Mzamiru amepata kura 115 sawa na asilimia 13.39.

Hii ni mara ya pili kwa Inonga kuchukua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki, Tuzo ya kwanza aliipata msimu uliopita.

Kufuatia ushindi huo Inonga atakabidhiwa Pesa Taslimu Shilingi 2,000, 000 na Tuzo kutoka kwa wadhamini wa Simba SC Kampuni Emirate Aluminium Profile ikiwa ni zawadi ya kuibuka mshindi.

Bilioni 313 zawanufaisha Wajasiriamali sekta ya Kilimo
Rais Young Africans atangaza vita Afrika