Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Hersi Said ametoa kauli ya kibabe kwa Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo katika kipindi hiki ambacho wanaelekea katika usajili wa msimu mpya 2023/24.

Young Africans imejipanga kuboresha kikosi chake kwa kufanya usajili wa baadhi ya wachezaji, huku ikiwa imeshatangaza kuwaacha Bernard Morroson, Dickson Ambundo na Tuisila Kisinda ambaye alikuwa klabuni hapo kwa mkopo akitokea RS Berkane ya Morocco.

Hersi amesema Uongozi wa Klabu hiyo umejipanga kufanya usajili mkubwa, licha ya maneno kuendelea katika baadhi ya vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii ambayo yanalenga kuidhohofisha Young Africans, hasa baada ya kuondoka kwa Kocha Mkuu Nasridden Nabi.

“Tunajua nini tunafanya sisi Kama Viongozi wa Young Africans licha ya maneno yote haya ambayo mnayaona kwenye mitandao, magazeti kuhusu sisi Viongozi na kushambuliwa kwa timu yetu. Tunajua ni kwa sababu tu ya watu fulani ambao hawapendi kuona tulipofika kwa sasa”

“Niwaombe tu kitu kimoja Kutoka kwa wanachama wetu na mashabiki wote wa Young Africans, tuendelee kuwa watulivu sisi Viongozi wao tunajua nini tunafanya, wanachama ambao watakaopata nafasi ya kuja kwenye mkutano jumamosi hii tunawaomba sana waje tuendelee kushirikiana kwa pamoja kuijenga timu hii na kufanya mkutano huu kama katiba yetu inavyotaka tufanye”

“Bado tupo Kwenye mabadiliko na haitoshi bado tunaendelea kuijenga timu kwa gharama yoyote ile ili Young Africans iwe imara leo na kesho. Mashabiki na Wanachama ninawaomba muwe watulivu muda wetu utapofika kila mtu atafurahi tumejipanga vyema sana.” Amesema Hersi Said

Rushwa ya ngono chanzo wasomi wasio na sifa
Wafanyakazi Serikalini Kenya, Tanzania wakosa ufahamu