Kiongozi wa mji wenye matukio lukuki ya uhalifu Gauteng, Panyaza Lesufi amethibitisha kwamba ofisi yake haikufaulu kupata kibali kutoka kwa Rais kumpa Kiernan Forbes “AKA” mazishi ya serikali.
Lesufi amesema Rais Ramaphosa alikataa ombi hilo la mchango wa kifedha na jinsi jimbo hilo lilivyotaka kumuenzi rapa huyo kwa kulifunika jeneza lake bendera ya Afrika Kusini na kupeperusha bendera nusu mlingoti.
Amesema, “mtu wa hadhi hii ya kimataifa ni lazima kuwe na aina fulani ya heshima na tunataka kufafanua kwamba haikuwa mchango wa kifedha, lakini ilikuwa heshima ya kufunika jeneza, kuhakikisha bendera inapepea nusu mlingoti na kusimamia mazishi.”
Hata hivyo, Lesufi amesema AKA atazikwa katika ukumbi uliojitenga wa Viongozi Mashujaa wa jamii Afrika ya Kusini, na familia yake awali ilisema nyota huyo atazikwa katika mazishi ya faragha, kesho jumamosi ya Februari 18, 2023 na ibada ya mazishi itafanywa hii leo, Februari 17, 2023.
Kiernan Forbes – AKA, aliuawa kwa risasi siku ya Ijumaa usiku (Februari 10, 2023), nje ya mkahawa wa Wish kwenye Barabara ya Florida huko Durban, KwaZulu-Natal, sambamba na rafiki yake, Tebello Motsoane ambaye ni mjasiriamali na mpishi maarufu.