Rapa kutoka Detroit nchini Marekani Sean Michael Leonard Anderson maarufu Big Sean ameendelea kuthibitisha kuwa na asili ya nchini Nigeria kwa asilimia takriban 60.
Big Sean alithibitisha uhalisia wake kupitia kipindi cha runinga ‘Drink Champs’ kinachorushwa na kituo cha Revolt Tv ikiwa ni mara ya pili baada ya mahojiano aliyoyafanya na The Vibe mapema mwaka 2018.
Awamu hii amedokeza kwa undani baada ya kuulizwa kuhusu upande wa pili wa asili yake kulingana na muonekano wake, ndipo alipofafanua kwa kusema kuwa ana asili ya India kwa asilimia takriban 40, na kwa upande wa Nigeria uhalisia wake ukiwa ni wa asilimia 60.
“Nina asilimia kubwa ya uhalisia wa Nigeria, nina asilimia 60 ya Nigeria, kwa kiasi kikubwa kwa mujibu wa historia, na kiasi kidogo nina asili ya India, babu yangu alikuwa kama muhindi halisi.” alisema Sean.
Big Sean, si msanii wa kwanza kutoka nchini Marekani kuutaja uhalisia wake wa kistoria wenye kumuhusisha na nchi za Afrika hasa Nigeria, ikumbukwe rapa Lil wayne naye mnamo mwaka 2020 kupitia kipindi cha ‘Drink Champs’
Aliwaambiwa watangazaji wa kipindi hicho “Mimi nina asilimia 53 ya asili ya Nigeria, na nililazimika kwenda Nigeria kupaona mahali hapo ambapo ni nyumbani.”