Mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, amesema yeye na wachezaji wenzake wanapaswa kuwa kitu kimoja katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Msimu huu 2023/24, Man United imekuwa na wakati mgumu katika kusaka matokeo mazuri ambapo hadi sasa, imepoteza mechi nne kati ya saba za Premier League.
Timu hiyo pia haina pointi katika Kundi A la Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kupoteza mechi mbili ilizocheza, ikifungwa 4-3 na Bayern Munich, kisha 2-3 nyumbani dhidi ya Galatasaray.
“Kwa sasa hatufanyi vizuri vya kutosha, tumekuwa tukiruhusu mabao pindi tunapofunga, tutakwenda kulijadili hilo.
“Kwa kweli ni kipindi kigumu sasa, lakini tunahitaji kushikamana na hiyo ndiyo njia pekee tunayoweza kutoka katika kipindi hiki,” alisema mshambuliaji huyo.