Hatua ya Pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), inaanza rasmi kesho Jumatano Desemba 20, 2017 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), michezo ya kesho Desemba 20, mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale y Songea na KMC ya Kinondoni; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador ya Kahama na JKT Oljoro ya Manyara; Boma FC ya Mbeya na Ndanda ya Mtwara; Mvuvumwa ya Kigoma ingawa kwa sasa imeweka maskani yake Dar es Salaam na JKT Ruvu ya Dar es Salaam; Abajalo ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya wakati Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita.

Desemba 21, 2017 Mshikamano ya Dar es Salaam itacheza na Polisi Tanzania ya Morogoro; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.

Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.

Mchezo kati ya Simba na Green Warriors utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.

Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.

Desemba 24, 2017 Young Africans itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Singida Utd wajiwekea lengo Mapinduzi Cup
Dkt. Mpango akaribisha wawekezaji kutoka Norway