Ray C ameamua kuwasaka waliokuwa mashabiki wake na kuchota mashabiki wapya katika eneo la Afrika Mashariki, kwa kufanya ziara.

Mwimbaji huyo aliyebatizwa jina la ‘Kiuno Bila Mfupa’ mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa uwezo wake mkubwa wa kukitumia kiuno chake awapo jukwaani, amesema kuwa ametembelea vyombo vya habari Afrika Mashariki kuutangaza wimbo wake mpya ‘Umenimaliza’ unaotambulisha kurejea kwake.

“Nimetembelea Uganda, Rwanda na sasa nipo Burundi wamenipokea vizuri nimefanya appearance (muonekano maalum) kama tatu kwenye klabu za usiku, kila sehemu wanaimba ‘Umenimaliza’,” Ray C aliiambia Clouds FM.

“Unajua huku [Burundi] watu wanajua Kiswahili. Radio zinapiga sana nyimbo za Bongo Fleva na watu wanakubali,”aliongeza.

Mwimbaji huyo alikumbuka mara ya mwisho kufika nchini Burundi, miaka mitano iliyopita alipofanya tamasha moja na 2Face kutoka nchini Nigeria.

Ray C amerejea rasmi kwenye ulingo wa Bongo Fleva baada ya miaka mingi ya mapambano ya kujinasua kwenye janga la matumizi ya madawa ya kulevya.

Q Boy awafungukia wanaosema hajui kuimba
Picha za Young Dee na Amber Lulu zamkosanisha na mama yake