Q Boy Msafi amewatolea uvivu wanaokosoa uwezo wake wa kuimba wakidai ni bora abaki kwenye upande wa kuwavalisha wasanii.

Msanii huyo ambaye kabla hajaingia kwenye muziki alifahamika kama mbunifu wa mavazi wa msanii Diamond, amesema maneno hayo yanamfanya aongeze juhudi katika kazi zake za muziki.

Ameiambia East Africa Television kuwa hakuna mtu anayeweza kuhukumu uwezo wake wa kuimba zaidi ya watayarishaji wa muziki ambao amefanya nao kazi.

“Mimi nina imani anayejua kama najua kuimba ni producer (mtayarishaji) ninayefanya naye kazi. Nina ma-producer (watayarishaji) kama watatu, hao ndiyo wanaoweza kusema najua au sijui,” alisema.

“Mimi nachukulia kama changamoto. Ujue ukiwa unatafuta riziki yako maneno kama hayo hayawezi kukosa,” Q Boy aliongeza.

Msanii huyo alianza kufahamika kwa mashabiki wengi wa muziki baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Mugachelele’ aliowashirikisha Shetta na Ray Vany.

Karim Mostafa Benzema hadi 2021
Ray C aizunguka Afrika Mashariki kuwasaka watu wake