Mwanamuziki Rayvanny ambaye anafahamika kama msanii anayesimamiwa na record label ya WCB ameibua maswali kwa mashabiki zake baada ya kuuondoa wasifu wake kuwa chini ya WCB, ambayo ndio record label iliyomtambulisha rasmi kwenye muziki.

Suala hilo limeibua mjadala mkubwa kufuatia kuwepo kwa fununu za nyota huyo kujiengua na label hiyo zilizoanza kusambaa kwa kasi tangu mapema mwaka jana 2021 baada ya Rayvanny kufungua Label anayoimiliki ya ‘Next level Music’.

Licha ya kuwa mara kadhaa Rayvanny alikanusha uvumi huo hasa kwa kubainisha kuwa ni suala la kawaida kwa msanii kuwa chini ya record label nyingine hali ya kuwa naye ni mmiliki wa label yake binafsi.

Ukiachilia mbali kitendo cha yeye kuuondoa wasifu huo wenye kuthibitisha kuwa chini ya WCB, takribani mwezi mmoja uliopita mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye ndio mmliki wa Label hiyo, katika mahojiamo yake na kituo cha Wasafi Radio aliweka wazi msimamo wake kuhusu uvumi juu ya hatma ya Rayvanny na WCB.

“Hizo issue za Rayvann hakuna kitu kama hicho, na ikifikia hivyo haiwezi kuwa tatizo, kwanza mimi namsifu kitu kimoja, Rayvann sio mwehu wala sio mjinga wa kuambiwa maneno. Kwa sababu unapokuwa wasafi unaambiwa maneno mengi sana, Rayvanny ana heshima sana.

Siku ukisikia Rayvanny anatoka Wasafi siamini kama unaweza kusikia anatoka kiuwendawazimu haiwezekani,” alisema Diamond akijibu swali la mtangazaji lil ommy.

Rayvanny kwa sasa anamiliki Record Label ya Next level Music ambapo ameshawekeana mikataba na wasanii kadhaa wanaochipukia.

Kocha wa Orlando Pirates amkera Haji Manara, awapa somo Simba SC
Kocha orlando aondoka Bongo shingo upande