Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge, amefanya ziara ya kushtukiza kwa mkandarasi wa soko la Tandale ili kujiridhisha kama anatekeleza maagizo ya kufanya kazi masaa 24 kwa siku.
RC kunenge amefanya ziara hiyo usiku wa kuamkia leo Desemba 22, 2020 baada ya siku mbili kupita tangu alipotoa agizo kwa mkandarasi huyo kufunga taa za usiku ili aweze kufanya kazi masaa 24.
Sambamba na kufanya kazi masaa 24 pia alimtaka mkandarasi huyo kuongeza idadi ya vibarua wa ujenzi ili amalize ujenzi kwa wakati.
Baada ya utekelezaji wa mkandarasi kufuata maagizo ya RC, Kunenge ameendelea kumsisitiza mkandarasi huyo kuhakikisha mradi huo unaisha kabla ya April, 2021.
Hata hivyo Kunenge ametoa tahadhari kwa wandarasi wote wanaotekeleza miradi jijini Dar es Salaam kuzingatia mikataba yao kwa kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati.