Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewapiga marufuku wakurugenzi wa halmashauri kutoka nje ya mkoa hadi watakapowasilisha ofisini kwake taarifa za maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda

Ametoa agizo hilo, hii leo wakati wa kikao maalum cha baraza la Madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela cha kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16

Amesema kuwa amepokea barua za ruhusa kutoka kwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za kutaka kwenda kwenye ziara mkoani Dodoma na kwamba amewazuia mpaka watakapowasilisha taarifa za utekelezaji wa sera ya viwanda katika maneo yao.

“Leo ninapambana na Wakurugenzi nimewanyima ruhusa, nimewaambia hakuna kutoka nje ya mkoa huu mpaka waniwasilishie taarifa za maeneo waliyotenga ya viwanda, mmechagua viwanda gani katika halmashauri yenu, maeneo hayo yapo wapi, yamepimwa au hayajapimwa, ripoti hiyo bado sijaipata,” amesema Makalla

Hata hivyo, Makalla ameongeza kuwa ameona awanyime ruhusa Wakurugenzi hao ya kusafiri kwenda ziara mkoani Dodoma mpaka watakapo kabidhi ripoti hiyo ofisini kwake.

 

 

Serikali yawafunda mawaziri wa Afya wa Afrika
Fid Q ajitosa kuwapatanisha Diamond na Ali Kiba