Rais Magufuli amezuia bomoabomoa nyumba zaidi ya 300 zilizojengwa kwenye Bonde la Msimbazi, hayo yamewakilishwa leo na Mkuu wa Mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alipotembelea eneo la bomoabomoa bonde la Msimbazi na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ishu ya bomoabomoa katika eneo hilo.
RC Makonda amewatoa wasiwasi wananchi ambao wamekuwa na hofu baada ya kuambiwa watabomolewa nyumba zao amewahakikishia kuwa hakuna atakayewabomolea nyumba zao.
”Nawaomba tujiepushe na sehemu hatarishi, kila kinachofanywa na Serikali ni kwa ajili ya kuwaokoa wananchi. Hakuna mtu atakayewabomolea nyumba zenu, hata Rais aliniambia hamkumchagua ili awabomolee nyumba zenu.
-
Wazazi wajawa hofu, watoto watano watekwa
-
Msigwa alalamikia Serikali awaombea kifuta jasho wenye vyeti feki
“Tulikubaliana na Rais kuwa nyinyi mjiepushe kujenga kiholela na kwenye maeneo hatarishi na mfuate utaratibu.” – RC Makonda.