Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewaonya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri kuacha mara moja kuwawekea vikwazo Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) kutimiza majukumu yao.
Ameyasema hayo mjini Tabora kwenye kikao kazi cha Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) wa mkoani humo wakati akijibu malalamiko yaliyotoka kwa Mawakala hao dhidi ya watendaji wa Halmashauri kuwakwamisha.
Amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji yoyote atakayewakwamisha Watumishi hao ajue amewadharau viongozi wa juu waliowatuma kazi Mameneja hao ya kuwaboreshea barabara wananchi wa vijijini na kwa nafasi yake hayuko tayari kuona hilo linatokea.
Aidha, baadhi ya vikwazo ni pamoja na kunyimwa magari na wanapopata magari wanang’anywa madreva wanaokuwa wamepangiwa kuwahudumia na wakati mwingine kutopangiwa maeneo ya kuendeshea shughuli zao za kiofisi.
-
RC Makonda awatoa hofu wananchi kuhusu bomoabomoa
-
Twaweza yatoa ripoti kuhusu upungufu wa muda wa kumwona daktari
-
HESLB yatoa nyongeza ya muda kwa waombaji mkopo elimu ya juu
Hata hivyo, kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani Tabora, Mhandisi Damian Ndabalinze amewashauri Mameneja wa TARURA kuwa milango iko wazi wakihitaji msaada wasisite kuwaomba ushauri ili waweze kutekeleza kazi kwa kiwango bora na kinacholingana na fedha.