Bodi ya Mkopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu HESLB imeongeza siku saba kwa wanafunzi wote wanaofanya maombi ya mkopo kwa wanaojiunga na elimu ya juu.

Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, HESLB Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4.

Mkurugenzi huyo amesema hadi kufikia jana waombaji 49282 tayari wamekwisha ingiza taarifa zao mtandaoni kuomba mkopo na waliokamilisha maombi hayo ni 15,473.

Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti na kukamilisha taratibu za uombaji mkopo.

 

“Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema.

RC Tabora awaweka kikaangoni Wakurugenzi
Twaweza yatoa ripoti kuhusu upungufu wa muda wa kumwona daktari