Wakala wa nishati Vijijini – REA, imejipanga kutekeleza Mradi wa kusambaza mitungi ya gesi ya kupikia 71,000 kwa utaratibu wa utoaji ruzuku, yenye thamani ya shilingi 3 bilioni, pamoja na majiko banifu 200,000 katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza na Waandishi wa habari hii leo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema kwa mwaka 2023/24, shilingi 10 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha mradi huo.

Amesema, usambazaji huo wa gesi utafanyika katikia Mikoa ya Mtwara, Lindi na Pwani (Pembezoni mwa Bomba Kuu la kusafirisha Gesi Asilia), na utaihusisha REA na TPDC ambapo jumla ya shilingi 20 bilioni zinatarajiwa kutumika katika mradi huo.

Amesema, “mradi huu pia utahusisha ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia (CNG) lenye urefu wa kilomita 44.4 ambapo ni kuanzia Mnazi Mmoja mpaka Lindi na kilomita 22.9 Mkuranga – Pwani. Serikali kupitia REA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imetenga Dola Milioni 6 kwa ajili ya mradi wa usambazaji wa majiko banifu ya kupikia.

Takribani Majiko 200,000 yanatarajiwa kusambazwa katika maeneo mbali mbali ya vijijini na vijiji miji Tanzania bara kwa engo la ukuza na kuboresha upatikanaji wa nishati safi ya kupikiaambapo kwasasa Wakala upo kwenye mchakato wa uandaaji wa taratibu na kanuni za utoaji wa ruzuku hizo.

Polisi wakamata Dawa za kulevya, Pombe haramu
Museveni aishukia tena Benki ya Dunia