Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewaasa vijana 136 walioajiriwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), nafasi za Waratibu Miradi ya Umeme Vijijini kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi, ili kulinda imani iliyooneshwa na Serikali juu yao.

Makamba ameyasema hayo jijini Dodoma, nankuwataka vijana hao 136 kwenda kuwatendea haki wananchi walengwa ambao ni wa maeneo ya vijijini nchi nzima, kwa kuhakikisha wanafikiwa na huduma ya umeme.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akizungumza wakati wa mkutano huo.

“Wote waliotuma maombi walikuwa na vigezo lakini kutokana na nafasi zilizohitajika kuwa ni 136, ndiyo maana wachache wenu kutoka kundi hilo mkabahatika ichukulieni fursa hii adhimu kuchapa kazi na kudhihirisha hatukufanya makosa kuwachagua,” amesisitiza Waziri Makamba.

Aidha, Waziri Makamba amesema kazi ya kupeleka umeme vijijini inaendelea vizuri ambapo hadi sasa takribani asilimia 80 ya vijiji vyote Tanzania Bara vimeshafikiwa na umeme, lakini pamoja na takwimu hizo nzuri, kumekuwepo na uchelewaji wa kupeleka nishati hiyo kwa baadhi ya vijiji, kutokana na usimamizi usiokidhi.

EWURA yatangaza bei za mafuta, Petroli yapaa
Tanzania, WB zasaini mkopo nafuu, msaada Trilioni 1.333