Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini, zitakazoanza kutumika kuanzia hii leo Jumatano, Machi 1, 2023 huku bei hizo zikionesha kupanda.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule imeeleza kuwa kwa Machi, 2023 bei za rejareja za mafuta ya Petroli imepanda kwa Sh. 149/ lita, Dizeli Sh. 25/ lita na Mafuta ya Taa Sh. 37/ lita kwa mafuta yaliyopokelewa kwa bandari ya Dar es Salaam ikilinganishwa na toleo la Februari 1.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule.

Amesema, “EWURA inapenda kuukumbusha umma kuwa bei za kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli kwa eneo husika, inapatikana pia kwa kupiga namba *150*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.”

Kwa mujibu wa sheria ya Mafyta ya mwaka 2015 kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta zitaendelea kupangwa na soko na EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei za kikomo za mafuta, zikilenga kuwasaidia wadau kufanya maamuzi sahihi ya manunuzi ya bidhaa hiyo.

Kocha mpya Stars apewa masharti mazito
Vijana wa REA wapewa darasa la ufanisi