Real Madrid ina mpango wa kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa na Klabu ya Paris St-Germain Kylian Mbappe lakini haipo tayari kutoa ada ya uhamisho.

Madrid inaamini ili kumpata Mbappe itagharimu Pauni 300 milioni jambo ambalo ni gumu kwao, hivyo inataka kusubiri hadi mkataba wake utakapomalizika ili kumsajili akiwa huru.

Mbappe amesaini mkataba mpya katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi na mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025.

Kabla ya kusaini mkataba mpya na PSG, Madrid ilikuwa na matumaini ya kumpata staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini ilishindwa baada PSG kuweka mpunga mrefu mezani.

Tangu kuanza kwa msimu huu 2022/23 Mbappe amecheza mechi 40 za michuano yote, amefunga mabao manane na kutoa asisti nne.

Balake kuendelea kupeta Simba SC
Vifo watu 201: Ruto akiri udhaifu wa vyombo vya usalama