Mashirika ya kiraia mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC yamesema watu zaidi ya 60 wameuawa katika kipindi cha wiki moja kutokana na mashambulio ya makundi ya waasi.
Mashirika hayo, yanasema mapigano yalizuka Jumapili ya wiki iliyopita kwenye mji wa Ituri, baada ya kuuawa kwa mwalimu wa jamii ya Lendu na hali iliyopelekea wapiganaji wa Codeco wanatetea jamii ya Hema kulipiza kisasi.
Hema na Lendu zimekuwa na mgogoro wa muda mrefu ambao hadi sasa umesababisha vifo vya mamia ya watu kati ya m,waka 1999 na 2003 kabla ya kutumwa kwa vikosi vya kimataifa kudhibiti mauaji yaliyokuwa yanatokea.
Jumatano Januarin 11, i2023 kuliripotiwa mashambulio mengine ya kusini mwa mji wa Ituri, ambako watu kadhaa waliuawa na waasi wanaodaiwa kuwa ni wa ADF huku shambulio jingine la waasi wa ADF liliripotiwa kutekelezwa siku iliyofuata, ambapo miili ya watu 21 ilipatikana kaskazini mwa
Riiuuupoti za umoja wa mataifa zaidi ya makundi ya waasi 120 yanafanya shughuli zao mashariki mwa DRC, mengi yakipigania kuchukua maeneo yenye utajiri wa rasilimali ikiwemo madini.