Nepal inaomboleza vifo vya watu 67, vilivyotokea kwa ajali ya Ndege ambayo inatajwa kuwa ni mbaya kuwahi kutokea nchini humo, kwa kipindi cha miaka 30.

Serikali ya Nepal, imetangaza kuanza kwa uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo, iliyotokea Januari 15, 2023 wakati ndege hiyo ikitoka mji wa Kathmandu kuelekea mji wa kitalii wa Pokhara na kuanguka wakati ikikaribia kutua uwanja ndege.

Raia na waokoaji wakiwa eneo la ajali ya ndege nchini Nepal. Picha ya Krishna Mani Baral/ AP.

Shughuli za kutafuta miili ya abiria ilisitishwa jana kutokana na giza, na sasa asubuhi hii ya Januaru 16, 2023 mamia ya wanajeshi wa Nepal wanaendelea na utafutaji huku chanzo cha ajali hiyo, kikiwa bado hakijafahamika.

Nchi ya Nepal, ina historia mbaya ya kushuhudia ajali kama hizo za ndege kutokana na kile kinachoelezwa kuwa na miundo mbinu mibaya ya viwanja na kingo za ndege kuzungukwa kwa milima.

Metacha Mnata awaomba radhi Wananchi
Singida Big Stars yafanya mabadiliko