Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amekanusha uvumi wa kuwakataa Makocha wazawa Juma Mgunda na Seleman Matola aliyewakuta Klabuni hapo.

Uvumi wa makocha hao kuwa kikaangoni, uliibuka baada ya kutambulishwa kwa Kocha Msaidizi kutoka Tunisia Ouanane Sellami, juzi Alhamis (Januari 19).

Kocha Robertinho amesema ataendelea kufanya kazi na Kocha Mgunda na mwenzake Matola kwa sababu anaamini wana msaada mkubwa katika shughuli zake za kila siku klabuni hapo.

Amesema ongozeko la Kocha Sallami, halina maana yoyote mbaya katika utendaji kazi katika Benchi la Ufundi la Simba SC, hivyo atafanya kazi na makocha wote watatu ambao wanaongeza ufanisi wa kiufundi.

“Makocha wazuri kama Matola na Mgunda uzoefu wao hapa Tanzania ni muhimu. siwezi kuacha kufanya nao kazi wanafahamu vitu vingi vya kiufundi nitaendelea kuwa nao,”

“Hakuna Kocha anayeweza kukataa kufanya kazi na makocha wazuri kama Mgunda na Matola, ila Sellami amekuja kuongeza nguvu ndani ya Benchi la Ufundi na tutafanya wote kwa pamoja.” amesema kocha huyo mwenye umri wa miaka 62

Robertinho ameongozana na makocha wake wasaidizi kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa 21 wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa kesho Jumapili (Januari 22), Uwanja wa Jamhuri

Wafurahia sheria ya mpya 30% ya ajira kwa Wanawake
Wanawake, watoto waliotekwa waachiliwa huru