Kocha msaidizi wa Manchester City, Rodolfo Borrell amefikia maamuzi magumu ya kuachana na mabingwa hao wa Barani Ulaya baada ya kupata mchongo mwingine wa kuwa mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Austin FC.
Mhispania huyo alijiunga na City kutoka Liverpool Mwaka 2014, kama Mkurugenzi wa ufundi wa kimataifa, kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa makocha wa akademi hiyo na kisha kujiunga na timu ya nyuma ya Pep Guardiola.
Borrell aliteuliwa kuwa meneja msaidizi kabla ya msimu uliopita, ambao ulishuhudia.
City wakishinda Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu England na Kombe la FA, huku akiwa ni msaidizi wa pili wa Guardiola kuondoka msimu huu wa joto kufuatia Enzo Maresca kuteuliwa kama kocha wa Leicester mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa soka wa Manchester City, Txiki Begiristain alisema: “Amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.
“Mara nyingi hata kocha mkuu Pep Guardiola amekuwa Akizungumzia jinsi timu yake ya makocha imekuwa. muhimu katika kumsaidia yeye na timu kufikia kile tulichonacho. Rodolfo bila shaka, amekuwa sehemu kubwa ya hilo wakati alipokuwa Manchester City.
“Nina imani kabisa kwamba atakuwa rasilimali kubwa kwa Austin FC na kandanda ya Marekani.”