Gwiji wa soka nchini England Wayne Rooney ameachana na kazi ya ukocha katika klabu ya Ligi Kuu ya Marekani ya DC United by kwa makubaliano maalum baada ya timu yake kushindwa mchezo wa mtoano wa Kombe la MLS.
Mchezaji huyo anayeshikilia rekodi ya Manchester United ya kufunga mabao mengi alichukua jukumu la kuifundisha timu hiyo yenye maskani yake jijini Washington, D.C Julai mwaka 2022.
Awali alitumia miezi 18 katika klabu hiyo kama mchezaji kabla hajajiunga na Derby kama kocha mchezaji Januari mwaka 2020.
“Sasa ni muda sahihi. Nimefanya kila kitu kuiwezesha klabu hii kucheza mchujo, “alisema Roney mwenye umri wa miaka 37.
“Sio kitu kimoja kimetokea. Ni suala la muda tu.”
DC United ilishindwa mchezo wa mchujo kwa mwaka wa nne mfululizo licha ya juzi Jumamosi kushinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu wa kawaida wa mchezo dhidi ya New York City FC.
Tulizungumza na Wayne na alikubaliana kuwa ni jambo bora kwetu kuachana katika kipindi hiki, “alisema mtendaji mkuu wa DC United na mwenyekiti mwenza Jason Levien.
Tunafuraha kwa yale yote aliyofanya Wayne Rooney katika klabu yetu na katika mchezo wa soka katika taifa letu kwa ujumla, kwanza kama mchezaji wa DC United na nahodha na hivi karibuni kabisa kama kocha wetu.