Baadhi ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Nyakato Wilaya Bukoba Mkoani Kagera, wameshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea vyumba sita vya madarasa na mabweni mawili na matundu ya choo 8 ya vyoo, hali itakayo ondoa adha waliyokuwa wanaipata awali huku wakiahaidi kuongeza ufaulu.

Wameyazugumza hayo baada ya kutembelewa na mjumbe wa utekeleza wa umoja wa wanawake Tanzania UWT na Katibu wa Wabunge wanawake wa CCM wakati wa kukagua miradi iliyotelezwa katika shule hiyo iliyoghalimu zaidi ya milioni 400.

Awali, akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu kwenye shule hiyo Mjumbe wa UWT uchumi na mipango Taifa, Regina Zachwa amewahasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii hali itakayofanya kufikia malengo ya ndoto zao.

Mjumbe wa utekelezaji wa umoja wa wanawake Tanzania UWT na Katibu wa Wabunge wanawake wa CCM, Subura Mgaru amesema Rais Samia ameboresha miundombinu ambapo ujenzi wa madarasa elfu 15 mwaka 2021 na mwaka 2022 zaidi ya madarasa 8000 yamejengwa kwa mwaka 2023.

Rooney avunja mkataba DC United
Machifu waomba makumbusho ya Ufipa, Wamsimika Chongolo