Wayne Rooney yuko mbioni kuelekea katika jiji la Washington kufanyiwa vipimo vya afya na kumalizia hatua za mwisho za kujiunga na klabu ya DC United inayoshiriki katika ligi kuu ya soka ya Marekani.
Habari kutoka katika mtandao wa Sky Sport zinasema mshambuliaji huyo wa Everton pamoja na wakala wake Paul Stretford wanatarajia kuwasili Marekani katika jiji la Washington siku ya Alhamisi kukutana na wamiliki wa klabu ya D.C United.
Rooney alijiunga na klabu ya Everton mwaka jana mwezi Julai akitokea Manchester United na ameisadia Everton kumaliza msimu ikiwa katika nafasi ya 8 ikiwa na pointi 49 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza akiwa amepachika jumla ya mabao 10.
-
Everton yamkata Rooney mshahara wa wiki mbili
-
Unai Emery ateuliwa kuwa kocha mpya wa Arsenal
-
Neymar arejea dimbani, Rivaldo amtabiria ‘Ballon d’Or’
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza amekuwa katika mapumziko na familia yake tangu kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya na imeripotiwa kuwa tayari ameanza kutafuta nyumba ya kuishi maeneo ya kasikazini mwa Virginia Marekani.