Mshambuliaji wa timu ya taifa Brazil, Neymar ameanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake kujiandaa na michuano ya kombe la dunia inayotarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 14 mwezi Juni nchini Urusi.

Neymar amekuwa nje ya uwanja tangu mwezi Februari akiuguza majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia klabu yake ya Paris Saint-Germain wakati klabu hiyo ikimenyana na Olympique Marseille.

Nyota huyo ataiongoza Brazil katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya kombe la dunia, mchezo utakopigwa tarehe 17 mwezi Juni wakati Brazili itakapo kabiliana na Uswizi.

Wakati huo huo kumekuwa na taarifa zinazomuhusisha mshambuliaji huyo kutimkia katika klabu ya Real Madrid na gwiji wa zamani wa Barazil, Rivaldo amesema itakuwa rahisi kwa Neyamar kushinda tuzo ya ‘Ballon d’Or’ endapo ataenda Madrid au katika klabu nyingine ya Uingereza.

Kurejea kwa Neymar kunatoa matumaini kwa kikosi cha Brazil kufanya vizuri katika michuano ya kombe la dunia mwaka huu kwani katika michuano iliyopita ya mwaka 2014 Brazil hawakufanya vizuri.

Watu 9, Bar 3 mbaroni kwa kuvunja maadili ya Ramadhani
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Iran