Waliokuwa mabingwa wa Tanzania Bara, Young Africans wamezinduka na kupata ushindi wa kwanza baada ya kucheza michezo tisa bila ushindi.

Young Africans Wamezinduka kwa kuichapa Mbao FC bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni.

Bao pekee la Young Africans limefungwa na nahodha na kiungo wa mchezo wa leo, Thaban Kamusoko  kwa ‘free-kick’, nje kidogo ya eneo la 18 ya Mbao, baada ya beki Vincent Philipo kuunawa mpira katika harakati za kuokoa mashambulizi.

Matokeo hayo yanaifanya Young Africans kufikisha alama 51 ambazo zinawaweka katia nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 55, huku Mbao wakibaki nafasi ya 13 na alama 30.

Baada ya mchezo wa leo mfungaji wa bao pekee la Young Africans Thaban Kamusoko amesema kinachowaponza hadi wanakuwa hawafanyi vizuri kwa siku za karibuni ni uchovu unaotokana na kubanwa na ratiba.

Kamusoko pia amesema anaamini kuwa timu yake itapata ushindi kwenye mechi zake zote zilizobaki ili kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili.

Young Africans ina nafasi ya kushika nafasi ya pili endapo itashinda michezo miwili iliyosalia ambayo ni dhidi ya Ruvu Shooting Mei 25 na mchezo dhidi ya Azam FC utakaopigwa Jumatatu Mei 28, mwaka huu.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 23, 2018
TPBO, PST zamkera Waziri Mwakyembe