Klabu ya Mbeya City imekua klabu ya pili msimu huu wa 2017/18 kubadili mfumo wa uendeshwaji wake na kuingia katika mfumo wa kampuni.

Mbeya City wameingia katika mfumo mpya wakifuata nyayo za klabu ya Simba ambayo mwishoni mwa juma lililopita, wanachama wake waliazimia kwa kauli moja kubadilisha vipengele vya katiba yao, ili iendane na mfumo mpya wa uendeshaji.

Katibu mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe, hii leo amethibitisha kufanyika kwa mabadiliko ya kiuendeshaji ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makuu jijini Mbeya, kwa kutoa taarifa aliyoisambaza katika vyombo vya habari.

TAARIFA KWA UMMA

KLABU YA MBEYA CITY IMEKUWA KAMPUNI

Timu ya Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya jiji la Mbeya inayoshiriki ligi kuu ya Vodacom imebadirisha mfumo wake wa uendeshaji na sasa ni Kampuni.

Kampuni hii ambayo imesajiliwa na msajiri wa makampuni na biashara nchini BRELA chini ya sheria ya makampuni (Companies Act,2002) tarehe 26.01.2018 inaitwa MBEYA CITY FOOTBALL CLUB PUBLIC LIMITED COMPANY (Mbeya City FC PLC) kwa hati namba 140785 na imesajiliwa Posta Mbeya kwa anuani namba 663.

Kampuni hii ina matarajio ya kukusanya mtaji wa shilingi 100 Bilioni.

Katika mfumo huu Halmashauri ambaye ni mmiliki ataamua ni sehemu gani(asilimia) ya hisa atakazobaki nazo na zingine zitapelekwa kwenye soko la mitaji ili kutafuta wamiliki/wabia wengine. Hisa hizo zitakuwa wazi kwa watu wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Bodi ya wakurugenzi wa kampuni na menejimenti ya timu itaundwa upya baada ya wanahisa wote kupatikana.

Klabu ya Mbeya City inakuwa klabu ya kwanza katika historia ya Taifa letu kuingia katika mfumo huu wa kisasa katika uendeshaji wa vilabu vya mpira wa Miguu Duniani.

Lengo la mabadiriko haya ya kihistoria ni kufungua mlango wa kupata wabia watakaoweza kukuza mtaji wa kampuni ili kufanya uwekezaji mkubwa kwenye timu,kugharamia miradi itakayojikita katika maendeleo ya mpira wa Miguu na miradi mingine itakayochochea ukuaji wa uchumi wa kampuni na taifa kwa ujumla.

Klabu inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau na wananchi mbalimbali walioiunga mkono katika kipindi chote hicho toka timu imeanzishwa mwaka 2011 na inawakaribisha kumiliki klabu yao pendwa kupitia utaratibu wa HISA pindi taratibu za uuzwaji wa hisa hizo utakapokamilika mapema katika siku za usoni na  kuandikishwa katika Soko la Mitaji la Dar Es Salaam (DSE).

Imetolewa na

E.E.Kimbe

AFISA MTENDAJI MKUU

MBEYA CITY FC PLC

22.05.2018

TPBO, PST zamkera Waziri Mwakyembe
EXCLUSIVE: Nimepata bahati kubwa sana, nilikuwa navizia wakati huo- Prof. Kitila Mkumbo