Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa amepata bahati kubwa sana ya kuteuliwa na rais Dkt. Magufuli kuwa katika nafasi hiyo kwani wanaharakati wachache sana ambao hubahatika kuteuliwa na mkuu wa nchi.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo amesema kuwa tangu awali alikuwa anaivizia uteuzi.

Amesema kuwa mwanaharakati yeyote duniani hufanya shughuli zake kwa lengo moja tu la kutaka kupata uteuzi ili aweze kuingia serikalini au kwenda kuomba kura kwa wananchi aingie bungeni.

“Kwasasa nimepata bahati kubwa sana kuteuliwa na mkuu wa nchi rais Dkt. Magufuli, mwanzoni nilikuwa napiga kelele barabarani tu, lakini kwa sasa hautaniona tena napiga kelele hadharani, niko ndani tayari kwa hiyo shida za wananchi nilizokuwa nazipigia kelele sasa nazimaliza ndani kwa ndani,”amesema Prof. Mkumbo

Mbeya City Yafuata nyayo za Simba SC
Watu 65 wafariki dunia kwa joto kali