Utafiti uliofanywa nchini Marekani umegundua kuna aina kadhaa za kucha zenye muonekano mbalimbali ambapo kila muonekano unatabiri upungufu au ongezeko la kitu fulani katika mwili wa binadamu.

Aina ya Kwanza ni kucha zenye vidoti vidoti vyeupe, utafiti umebainisha kuwa mtu mwenye kucha zenye muonekano huu ana upungufu wa madini mwilini aina ya Calcium na Zinki, lakini pia vidoti huashiria ugonjwa wa Alegy, ugonjwa huu hutokea pale ambapo mwili kutokupatana na baadhi ya vitu au chakula matokeo yake ukikutana na vitu hivyo mwili humwaga sumu ambayo hudhuru eneo fulani la mwili lililokutana na kitu hiko ambapo wengine huwashwa na kuvimba, wengine hutoka vipele huku wengine hutokwa na vidonga au majipu kila mtu ana namna yake ambayo anaweza kudhurika na vitu ambavyo havipatani na mwili wake.

Related image

Aina ya pili ni kucha yenye mstari mweusi katikati, kucha aina hii huashiria ugonjwa wa kansa ujulikanao kama Melanoma, hii ni kansa ya ngozi, dalili hii ilielezwa na Profesa Sanchia Aranda ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kansa Australia.

Melanoma ni saratani ya ngozi inayoweza kugundulika kwa haraka zaidi na kusambaa kwa haraka zaidi, Saratani hii si tu hushambulia ngozi bali ina uwezo mkubwa wa kiushambulia viungo vingine ikiwemo mifupa.

 

Aina ya tatu ni aina ya kucha yenye alama nyeupe alama ya nusu mwezi mwanzoni mwa kucha, hii inaashiria mtu huyu ana mmeng’enyo mzuri wa chakula, mwilini pamoja na afya ya tezi za mwili.

 

Na aina ya nne ni kucha ambazo hazina alama ya nusu mwezi kucha hizi humaanisha mtu ana udhaifu na afya mbovu, Hii husababisha msongo wa mawazo, kubadilikabadilika kwa ”mood” ya mtu, kuongezeka uzito na kuwa na nywele nyepesi.

Related image

Na aina ya tano ni kucha yenye rangi ya njano ambapo kucha za rangi hiyo kuashiria kupatwa kwa fangasi.

Chukua tahadhari endapo utakuta una kucha za aina mojawapo hapo juu.

Video: Ni kweli kwamba nchi yetu ni masikini- Prof. Kitila Mkumbo
Rais RT ampongeza Mkurugenzi mpya MultiChoice