Jeshi la Magereza Nchini Tanzania limerejesha rasmi shughuli za kutembelea wafungwa, mahabusu na huduma mbalimbali kutoka magereza kuanzia Agosti Mosi zilizokuwa zimesitishwa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona nchini.
Msemaji wa Jeshi la Magereza SSP. Amina Kavirondo amesema huduma zimerejeshwa kutokana na kushuka kwa kasi maambukizi ya ugojnwa wa corona nchini, na kwa kuzingatia tamko la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuzitaka Taasisi za Serikali kurejea katika shughuli mbalimbali za utendaji.
Aidha Amina amewataka wageni wote wataokuwa wanafika gerezani kwa ajili ya kupata huduma kufuata kanuni na miongozo ya Jeshi la Magereza na Wizara ya Afya kwa mfungwa na mahabusu kutemembelewa na watu wasiozidi wawili kati ya jumamosi au jumapili, mazungumzo yasizidi dakika tano na wenye vibali vya kuleta chakula anaruhusiwa mtu mmoja.
SSP. Amina ameongaza kuwa wageni wote wanatakiwa kuvaa barakoa , kunawa mikono na maji tiririka na sabuni wanapoingia eneo la magereza na kuwa umbali wa mita moja.