Klabu ya Juventus imepewa adhabu ya kucheza mchezo mmoja bila sehemu ya jukwaa moja la mashabiki wao baada ya kumtusi kwa kejeli za kibaguzi mshambuliaji wa Inter Milan, Romelu Lukaku.

Lukaku alilengwa na mashabiki wa Juve kabla na baada ya kufunga Penati dakika ya tano ya muda ulioongezwa na kuwafanya Inter kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali ya Coppa Italia iliyochezwa Jumanne iliyopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alipewa kadi ya pili ya njano kwa kuweka vidole kwenye midomo yake ili kuwanyamazisha mashabiki hapo kwenye Uwanja wa Allianz.

Bodi ya Ligi Kuu Italia, Serie A, imetangaza Juve lazima wafunge jukwaa moja la Kusini kwa mchezo wao ujao wa ligi ya nyumbani, ambao ni dhidi ya Napoli utakaochezwa Aprili 23, mwaka huu.

Taarifa ilisema “wengi wa watazamaji 5,034” katika jukwaa hilo walikuwa wakitoa maeno ya ubaguzi wa rangi kwa Lukaku.

Lukaku bado atatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja katika mechi ya marudiano na Juve itakayochezwa Aprili 26, mwaka huu kwa kuonyeshwa kazi nyekundu.

Jean Baleke mchezaji bora Ligi Kuu
Solskjaer atajwa Club Brugge ya Ubelgiji