Naibu Rais wa Kenya, na mgombea Urais William Ruto (55), amesema atawatimua raia wa China waliopo nchin humo ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na wakenya iwapo atachaguliwa mwezi Agosti.
William Ruto, ameyasema hayo katika kongamano la kiuchumi nchii humo, huku Ubalozi wa China wa jijini Nairobi ukiwa bado haujajibu kuhusu kauli hiyo ya Ruto anayewania kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.
“Waacheni raia wa China wachome mahindi na kuuza simu za rununu, tutawarudisha wote katika nchi zao, shughuli hizi zote ni za Wakenya na msijali kuhusu wageni wanaofanya shughuli hizi tuna ndege za kutosha kuwatimua,” alisisitiza Ruto.
Ruto anayeonekana kama mtetezi wa watu wa uchui wa chini wenye rasilimali dhidi ya nasaba zinazotawala Kenya, amekuwa akikosoa sera za kiuchumi za Rais Kenyatta na akiahidi kufuta deni la nchi hiyo linalokadiriwa kufikia dola bilioni 70, iwapo atashinda uchaguzi huo wa mwezi Agosti.
China, ambayo ni mkopeshaji wa pili wa fedha nchini Kenya baada ya Benki ya Dunia na inafadhili miradi mbalimbali ya miundombinu ghali zaidi tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka wa 1963 ikiwemo njia ya treni inayounganisha mji wa bandari wa Mombasa hadi Naivasha katika Bonde la Ufa kupitia mji mkuu Nairobi.
Uwekezaji huo, umeambatana na kufurika kwa wafanyikazi wa China na kauli ya William Ruto imezua hisia tofauti mtandaoni kwa baadhi ya watu kusema anadhohofisha uhusiano wa nchi hizo ikizingatiwa kwamba Kenya ina deni la mabilioni ya China.
Wamesema, maamuzi ya Ruto yatapelekea kudhohofisha uhusiano huo na kuibua hoja zinazoweza kuifanya China kudai mikopo yaohuku wengine wakisimama na Roto katika pendekezo hilo.
Uchaguzi wa Urais Agosti 9, 2022 ukihusisha wabunge na viongozi wa mitaa, unakuja huku nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki ikikabiliwa na matatizo ya kiuchumi, yaliyosababishwa na janga la Uviko-19 na vita nchini Ukraine.