Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez amewashukuru Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kwa kuonyesha mapenzi na timu yao, katika kipindi hiki ambacho wanamaliza msimu pasina taji lolote la michuano ya Tanzania Bara waliyoshiriki.

Mashabiki na Wanachama wa Simba SC wamekua wakijitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa kuishangilia timu yao, na kuonyesha kuwa pamoja na wachezaji ambao walipambana tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Barbara ametoa shukurani hizo, baada ya Simba SC kucheza mchezo wake wa mwisho Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa msimu huu jana Alhamis (Juni 23).

“Hii inaonyesha Mashabiki na Wanachama wanaipenda timu yao kwa kiasi kikubwa, kama Uongozi tunawashukuru sana upendo wao, wamepambana sana kwa kuipa nguvu timu yao, leo (Jana) tumekamilisha michezo yetu kwa kucheza hapa.”

“Hata katika mchezo wetu wa mwisho kule Songea tutakua na jambo letu, hivyo Mashabiki na Wanachama wanapaswa kuendelea kuiunga mkono timu yao kwenye michezo miwili iliyosalia.” Amesema Barbara.

Simba SC itacheza mchezo wa Mzunguuko wa 29 mjini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine dhidi ya Tanzania Prisons na kisha itamaliza msimu wa 2021/22 kwa kupambana na Mbeya Kwanza FC mjini Songea mkoani Ruvuma katika Uwanja wa Majimaji.

Kifaru: Simba SC ina kiwango bora cha uchezaji
Ruto afikiria kuwatimua Wachina