Chuo kikuu cha Rwanda kimezindua mashine ya kwanza iliyotengenezwa nchini humo ambayo itawasaidia wagonjwa wa Covid 19 kupumua lengo likiwa ni kuitua serikali mzigo wa kuagiza mashine kama hizi kutoka nje.
Kwa mujibu wa DW Mashine hiyo inayomsaidia mgonjwa aliyeko mahututi kupumua wenyewe wanasema thamani yake ni dola elfu 10 za Marekani inaponunuliwa kutoka nchi za nje.
Hata hivyo mabingwa walioitengeneza wanasema kwamba kwa sasa kutokana na dunia kukabiliwa na tatizo la Covid-19 bei ya mashine hii imepanda hadi dola za Marekani elfu 20.
Naye Profesa Stephen Rulisa mkufunzi katika chuo kikuu Chuo hicho anasema licha ya kuongoza mchakato wa kuitengeneza mashine hiyo ni vijana wake walioitengeneza.
”Sisi tunawapa kazi ya kisayansi, tunawapa mawazo kama haya kisha wao hukaa kwenye maabara kama hapa na tunafurahi kwamba hatimaye wanafanya jambo kama hili,” amesema Profesa Rulisa.
Corona yawapandisha mume na mke kizimbani
Costa Uwitone, mmoja wa wanafunzi walioshiriki kutengeneza amesema kuwa wanachohitaji ni ushirikiano wa ngazi zote ili tutengeneza mashine nyingi na kuziweka sokoni kwa sababu zinahitajika kwa wingi
Mpaka hivi sasa Rwanda ina visa 147 vya corona huku watu 80 wakiwa wamepona na 67 wakiendelea kutibiwa hospitali.